Friday, 11 December 2009

Wajumbe wa Deni la Mabadiliko ya Tabia Nchi

Unakutana nao karibu kila kona unayokatiza. Ni vijana wadogo, lakini wakipita karibu na uliposimama huwezi kuacha kuwatazama, wanakufanya ulazimike kushirikiana nao katika kile wanachofanya. Wamejibatiza jina la Climate Debt Agents. Hawa ni vijana toka katika nchi kadha za Kiafrika ambao wapo ha Kopenhagen kupiga mbiu ya kuyataka mataifa makubwa kulipa deni lao juu ya uharibifu mkubwa wa mazingira ambayo wamefanya kwa dunia. (kutoka kushoto: Edith January, Zimbabwe; Rachel Kessi, Joyce Anjiri, Tanzania)

Mwandishi maarufu wa masula ya mabidiliko ya tabia nchi, Naomi Klein, alisifu juhudi zao wakati alipokuwa akitoa mada jana katika mkutano wa watu wa ‘Klima’. Unaweza kusoma habari zao zaidi katika mtandao unaokwenda kwa jina la www.climatedebtagents.com (Adrian Nzamba, Tanzania; Bob Sankofa)

No comments:

Post a Comment